Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Tukio muhimu la ufunguzi wa Darul- Qur'an inayobeba Jina la Zainul - A'bidina (a.s) - Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), limefanyika Jijini Mwanza, Tanzania likisimamiwa na Samahat Sheikh Zaydu Kishama.
Chuo hiki cha Darul-Qur'an kimefunguliwa Jijini Mwanza kwa malengo ya kufundisha kujua kusoma Qur'an Tukufu, Kuhifadhi Qur'an Tukufu, na kutoa elimu ya Tafsiri ya Qur'an Tukufu. Pia Kituo hiki cha Qur'an Tukufu kitajikita katika kufundisha Lugha ya Kiarabu (kuandika na kuongea). Waislamu wa madhehebu mbalimbali, Viongozi mbalimbali wa Serikali, Taasisi mbalimbali, Baraza Kuu la Waisamu Tanzania (BAKTWA) ni miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria katika Tukio hili muhimu na la kihistoria Jijini Mwanza, linalofungamana na Uhuishaji, Udumishaji na Uimarishaji wa Elimu na Maarifa ya Qur'an Tukufu.
Sheikh Zaydu Kishama, Msimamizi wa Darul - Qur'an Zainul - A'bidina (a.s) Jijini Mwanza, akimkabidhi zawadi ya Qur'an Tukufu Sheikh Fadhil, mjumbe wa Baraza la Masheikh Mkoa wa Mwanza, na Kadhi wa Wilaya ya Nyamagana, ambaye katika tukio hili ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi akimuwakilisha Samahat Sheikh Hassan Kabeke, Sheikh wa Mkoa wa Mwanza - BAKWATA.
Katika picha ni Sheikh Awadhi, Msomaji bingwa wa Qur'an Tukufu ndani ya Mwanza, Tanzania.
Pichani ni Sheikh Muhsin, Hafidhi Maarufu wa Qur'an Tukufu Jijini Mwanza, na amehifadhi Qur'an Tukufu yote kichwani.
Alihudhuria tukio hili la Ufunguzi wa Darul - Qur'an Zainul Abidina (as) na kuzikonga nyoyo za waumini kwa kuwapa kisomo kizuri cha Aya mbalimbali za Qur'an Tukufu.
Viongozi wa Serikali na Dini kwa pamoja wakikagua Mazingira ya Chuo hiki cha Qur'an Tukufu, Madarasa na Mabweni.
Mwenye Kanzu nyeusi katika picha ni: Sheikh Masasi, Katibu wa Baraza la Masheikh, Mkoa wa Mwanza.
Your Comment